Matthew 27:11-14

11 aWakati huo Isa akiwa amesimama mbele ya mtawala, mtawala akamuuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?”

Isa akasema, “Wewe wasema hivyo.”

12 bLakini viongozi wa makuhani na wazee walipomshtaki, hakujibu neno. 13 cNdipo Pilato akamuuliza, “Je, husikii ni mambo mangapi wanayokushtaki nayo?” 14 dLakini Isa hakumjibu hata kwa shtaka moja, kiasi kwamba mtawala alishangaa sana.

Copyright information for SwhKC